WATU 18 WAFARIKI KWA AJALI YA NDEGE, RUBANI ANUSURIKA – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Watu 18 wameripotiwa kufariki dunia katika mji wa Kathmandu nchini Nepal kutokana na ajali ya ndege ya kampuni ya Saurya Airlines iliyotokea Jumatano tarehe 24 Julai 2024, ambayo ilianguka kisha kuwaka moto.

 

Kulingana na vyombo mbalimbali vya habari, mtu mmoja pekee ambaye ni rubani alitoka salama kwenye ajali hiyo na ameelezwa kuendelea kupatiwa matibabu hospitalini.

 

 

Inaelezwa kuwa ndege iliyopata ajali ilianza safari zake kutoka uwanja wa Kimataifa Tribhuvan kuelekea kituo kinachotambulika zaidi kwa vivutio vya utalii cha Pokhara ikiwa na viongozi na wasaidizi wao ambapo kabla ya kufika katika kituo kilichopangwa ilipata ajali na kusababisha umauti wa watu hao na kujeruhi mmoja.

 

 

Bado mamlaka rasmi hazijatoa taarifa rasmi juu ya sababu au chanzo cha ajali hiyo kwa kuwa ndege hiyo ilionekana na kutambulika baada tu ya kuwaka moto.

 

 

Related Posts