MSIMU wa tatu wa Tamasha la “Grand Gala Dance” limechukua sura mpya bendi 04 kupanda Jukwaani mwezi Agosti 03,2024 katika ukumbi wa Superdom Masaki Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Wanahabari Leo Julai 24, 2024 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Chocolate Princess Iimited Mboni Masimba amesema kwa kutambua mchango mkubwa wa Muziki wa dansi uongozi wa Kampuni imeamua kuwaletea mashabiki wa muziki wa dansi bendi 04 ikiwemo Bendi ya Twangapepeta,FM Academia, Tukuyu Sound,Malaika bendi chini ya Uongozi wa Rais wa Masauti Christian Bella.
“Bendi hizi 04 tunajua uwezo wao hivyo ni bahati kubwa na tuna uhakika Mashabiki wa muziki wa dansi nchini wataipokea kwa ukubwa na watakongwa nyoyo huku Twangapepeta, Tukuyu sound,FM Academia pamoja na Malaika bendi.
Hata hivyo ametoa Pongezi kwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa Kuhakikisha Tamasha hili linafanyika kila Mwaka kwa ufanisi Mkubwa zaidi huku akimtaja mgeni rasmi kwa Mwaka huu anatarajiwa kuwa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Damas Ndumbaro.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka CRDB Sauda Makila amesema Kwa upande wa Benki hiyo wamejipanga kutoa huduma za kifedha kwa wadau watakaokuwepo katika Tamasha hilo .
“Tunatambua kuwa kwenye mkusanyiko wa watu hasa kwenye Matamasha huduma ya fedha haikosekani hivyo tumeona CRDB iwepo katika Tamasha la “Grand Gala Dance” kwa huduma ya Lipa hapa ili iwezo kuwa msaada kwa watu watakaohitaji huduma ya vyakula na vinywaji. “
Pia ameongeza kuwa CRDB itawezesha huduma ya Kununua ticket ili kupunguza usumbufu wa kufika vituo vya ticket .
Nae Rais wa Bendi ya FM ACADEMIA Patcho Mwamba amethibitisha kuwepo Katika Tamasha na kutumbuiza ili kukonga nyoyo za Mashabiki wa Muziki wa dansi.
“Tamasha hili mahususi kwa ajili ya kutoa burudani kwa Mashabiki ambao wanatamani kupata burudani ya muziki wa dansi kutoka bendi tofauti tofauti eneo moja hivyo sisi kama FM Academia tutatoa burudani hatutokuwepo kwa ajili ya Mashindano.”
Mkurugenzi wa Kampuni ya Chocolate Princess Limited Mboni Masimba akizungumza na Wanahabari Leo Julai 24,2024 Jijini Dar es Salaam wakati akitangaza Msimu wa 03 wa Tamasha La “Grand Gala Dance ” itakayofanyika Agosti 03,2024 ukumbi wa Superdom Masaki Jijini Dar es Salaam ikipambwa na Bendi 04 ikiwemo Twangapepeta, Tukuyu sound, Malaika bendi pamoja Fm Academia