Alaf Yakabidhi Mabati Ya Sh. Milioni 35 MOI

Ofisa Mawasiliano na Uhusiano wa ALAF Limited (Tanzania), Theresia Mmasy (wa tatu kushoto) akipeana mkono na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo, Dkt. Antony Assey (wa pili kushoto) wakati akikabidhi msaada wa mabati yenye thamani ya milioni 35 kwa ili kusaidia ukarabati wa Kitengo Cha Wagonjwa wa Nje (OPD) na eneo la mapokezi. Wanaoshududia ni kushoto na Kulia ni watumishi wa MOI na ALAF.


Na Mwandishi Wetu

KATIKA  kuhakikisha Jamii inafaidika k2a kupata huduma nzuri, kampuni ya Mabati ya ALAF, Tanzania imekabidhi mabati yenye thamani ya Sh. 35 milioni kwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) ili kusaidia mradi wa ukarabati wa taasisi hiyo.

Akikabidhi msaada huo leo Julai 25,2024 Ofisa Mawasiliano na Uhusiano wa ALAF Theresia Mmasy amesema msaada ambao unalenga kusaidia Taasisi hiyo ya MOI kufanya ukarabati wa kitengo cha wagonjwa wa Nje (OPD) eneo la mapokezi ni sehemu ya mpango wa kampuni hiyo katika kusaidia jamii.

“Sisi ni sehemu ya jamii na nia yetu ni kuona watu, ambao pia ni wateja wetu, wanapata huduma bora ambazo zitawezeshwa na ukarabati huu,” amesema.

Aidha, Theresia ameipongeza MOI kwa kutekeleza mradi huo wa ukarabati ambao utawafanya wagonjwa wengi zaidi kutoka Tanzania nzima kuhudumiwa Kwa haraka.

“Tunaahidi kuendelea kuunga mkono miradi kama hii kwa manufaa ya jamii,” ameongezea.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Antony Assey ameishukuru ALAF Limited kwa mchango wake huo na kusema kwamba utasaidia kwa kiasi kikubwa katika ukarabati huo na kufanya Kitengo cha OPD pamoja na mapokezi kuwa vya kisasa zaidi.

“Msaada huu imekuja wakati mwafaka zaidi kwani tutahakikisha tunatoa huduma Bora zaidi mara ukarabati huu utakapokamilika,” amesema.

Pia Dkt Assey ametoa wito kwa makampuni mengine na mashirika kuiga mfano wa ALAF

Related Posts