CHUO Cha Bahari Dar es Salaam ni miongoni mwa taasisi mbalimbali za serikali na binafsi katika Maonesho ya Vyuo Vikuu Tanzania yanayoendelea katika viwanja vya Gombani – Pemba.
Maonesho hayo ni mfululizo wa maonesho ya vyuo vikuu yanayoandaliwa na kuratibiwa na NACTVET ambapo mwaka huu 2024 yalianzia jijini Arusha kufuatiwa Unguja na sasa kuhitimishwa katika kisiwa cha Pemba – viwanja vya Gombani.
DMI ikiongozwa na wataalam mbalimbali wa tasnia ya Bahari wapo mahiri kuelezea Kozi mbalimbali zitolewazo na DMI lakini pia pamoja na fursa zitokanazo na Bahari.
DMI katika Banda lao wamejipanga kutoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na usajili wa papo Kwa papo.
Karibu DMI chuo pekee chenye Kozi za kipekee nchini Tanzania na Afrika mashariki.