Geita kuandikisha wapiga kura wapya 299,672 uchaguzi mkuu

Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya wapatao 299,672 katika Daftari la Kudumu la wapiga kura ndani ya Mkoa wa Geita ikiwa ni sawa na Ongezeko la Asilimia 24.7, ya wapiga kura Milioni 1.2 ambao ni sawa na wapiga kura waliopo kwenye Daftari hilo.

Hayo yameelezwa katika Mkutano wa Tume huru na Wadau wa Uchaguzi katika kuboresha Daftari hilo la kudumu na Mkurugenzi wa Tume huru ya Uchaguzi Bw. Ramadhani Kailima ambapo amesema Idadi hiyo inaweza kuongezeka endapo kutakuwa na watu waliokuwa na sifa za kuandikishwa kwa mwaka 2019/ 2020.

“ Kwa nchi nzima tuna vituo 40,126 vya kuandikisha wapiga kura ambavyo vitatumika katika uboreshaji wa Daftari 2024 na vituo hivi 39,709 vipo Tanznaia bara na 417 vipo Zanzibar na hiili ni ongezeko la vituo 2,312 ikilinganishwa na vituo 37,814 vilivyotumika 2019/2020 , ” Mkurugenzi Kailima.

Mkurugenzi wa Tume huru ya Uchaguzi amesema Kuongezeka kwa idadi hiyo kunauwezesha Mkoa wa Geita kuwa na wapiga kura zaidi ya Milioni 1.5 katika uchaguzi mkuu ujao wa madiwani ,wabunge na Rais unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.

” Kwa mkoa wa Geita kutakuwa na vituo vya kuandikisha wapiga kura 1637 vitatumika mwaka huu uboreshaji wa Daftari la wapiga kura ikiwa na ongezeko la vituo 3068 kutoka vituo 1569 vilivyotumika mwaka 2019 / 2020 , ” Mkurugenzi Kailima.

Kailima amesema tayari tume imefanya maandalizi kwa kutambua vituo 1,637 vitakavyo tumika kwenye uboreshaji ambapo kwa mwaka huu vituo vipya 68 vimeongezeka kutoka vituo 1,569 zilivyotumika kwenye uboreshaji wa mwaka 2019/20.

Kailima amevitaka Vyama vya Siasa kutumia muda huu kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha na kuboresha taarifa zao ili wapate sifa ya kupiga kura badala ya kuanza kulalamika na kusababisha wadau waache kushiriki katika zoezi hilo.

Awali mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi Jaji Jacobs Mwambegele amesema mzunguko wa pili wa uboreshaji wa Daftrai la Kudumu la wapiga kura utajumuisha Mkoa wa Geita na Kagera ambapo utaanza Agosti 5 mpaka 11,2024 na vituo vitafunguliwa saa mbili asubuhi hadi saa 12 jioni.

Askofu Flavian Kassala wa Jimbo Katoliki Geita ameonyesha wasiwasi wake wa siku saba zilizotengwa kwa ajili ya kuboresha daftari kama zitaweza kuwaandikisha wote watakaojitokeza na kushauri kama zinaweza kuongezwa ikafanyika hivyo ili wale wenye sifa waweze kuandikishwa.

Related Posts