JELA MAISHA KULAWITI MWANAFUNZI WA DARASA LA NNE – MWANAHARAKATI MZALENDO

#HABARI Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakamani ya Wilaya Kigamboni MH. Josiah Kemilembe Julai 22,2024 amemuhukumu kifungo cha kwenda jela maisha mtuhumiwa Juma Hassan Maulid (21) mkazi wa Mwera Gezaulole Manispaa ya Kigamboni baada ya kupatikana na hatia ya kosa la Kulawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 10 mwanafunzi wa darasa la nne.

Awali imeelezwa Mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo mwezi Februari,2024 baada ya kumlaghai mtoto huyo kwa kumpa pipi ya kijiti na kufanikiwa kumlawiti.

Cc; Police Force Tz (Mtandao ‘X’)

Powered by @kobemotor @acbtanzania_ @vodacomtanzania @hisense_tanzania_official @betpawatanzania @wearekerry
#KonceptTvUpdates

Related Posts