Picha: Rais wa Zanzibar Dk Mwinyi ahudhuria maadhimisho ya siku ya Mashujaa Dodoma

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi leo tarehe: 25 Julai 2024 amehudhuria Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa katika Uwanja wa Mashujaa, Mji wa Serikali Mtumba Dodoma.

Tanzania huadhimisha Siku ya Kuwakumbuka Mashujaa waliopoteza maisha yao wakiutetea, kuupigania na kuulinda uhuru wa Tanzania kila ifikapo Julai 25 ya kila mwaka. Siku hii ya kuwakumbuka mashujaa huambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo dua na sala maalum ya kuwaombea mashujaa waliopoteza maisha na kuiombea amani nchi kutoka kwa viongozi wa dini. Pamoja na hayo hufanyika gwaride maalum kwa ajili ya mashujaa wetu.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Halikadhalika Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozo wa Serikali, Makamanda Wakuu, Vikosi vya Ulinzi na Usalama pamoja na Viongozi wa Dini.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

 

Related Posts