Rais na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ashiriki Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa katika Mji wa Serikali Mtumba Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiweka silaha za Asili (Mkuki Ngao) na shada la maua kwenye mnara wa Mashujaa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa. Maadhimisho hayo yamefanyika katika Uwanja wa Mashujaa uliopo kwenye Mji wa Serikali Mtumba Mkoani Dodoma tarehe 25 Julai, 2024.