Na Mwandishi Wetu.
Shule ya Msingi ya Mchepuo wa dini ya Kiislam ya Answaar iliyoko Kinondoni Studio Jijini Dar es Salaam imeipongeza serikali kwa sera ya Elimu kwa vitendo kwani inawasadia vijana kujiajiri.
Mwalimu wa Dini dini wa Shule hiyo Ramadhani Omary Lubuva anasema kuwa serikali imeweka sera ambayo itawawezesha vijana kujiajiri na hivyo kutokaa vijiweni baada ya kumaliza masomo yao katika hatua tofauti.
“Tunaipongeza serikali kwa hatua hiyo, ni jambo jema hata hapa shuleni kwetu tunafundisha vijana ujuzi tofauti tofauti kama vile ushonaji na masomo mengine ya Dini kwa Vitendo,” anasema.
Anasema kuwa shule yao imekuwa ikiwafundisha vijana kwa kufuata mtaala wa Wizara ya Elimu sanjari na elimu ya Dini ya Kiislam jambo ambalo limeifanya shule kuzalisha viongozi bora kabisa wenye hofu ya Mungu.
“Tuna wakuu wa Wilaya , Wataalam mbalimbali wa serikali waliopitia shuleni hapa na kwamba huko waliko wamekuwa viongozi bora sana kwani wana maadili pia wana hofu ya Mungu,” anasema.
Anafafanua kuwa wanafundisha vijana wa madhehebu mbalimbali kama vile Wakrito na wasio na dini hapa, wanaletwa na wazazi wao kwa lengo la kupata elimu yenye maadili mema,” anasema .
Anafafanua kuwa siyo rahisi kwa vijana wanaopita shuleni hapo kuwa wala rushwa au mafisadi kwani wanajifunza elimu ambayo inawapa hofu ya Mungu.Anatoa wito kwa wananchi kupeleka watoto shuleni hapo
Mwalimu wa Dini wa Shule Kiislam Ramadhan Omary Lubu