Timu ya Simba Queens imepangwa kundi B katika michuano ya kufuzu fainali za Afrika kwa Wanawake kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Timu tisa zimepangwa kwenye makundi mawili na bingwa wa michuano hiyo ataiwakilisha CECAFA kwenye mashindano ya Afrika.
Kundi B ambalo ndio Simba yumo lina timu zifuatazo: Simba Queens (Tanzania), PVP Buyenzi (Burundi), Kawempe Muslim (Uganda), Fad Djibouti (Djibouti) .
Michuano hiyo itaanza kutimua vumbi Agosti 17 na kumalizika Septemba 4 katika mji wa Addis.