VITAL’O WAHAMISHIA MECHI YAO NA YANGA, AZAM COMPLEX – MWANAHARAKATI MZALENDO

Klabu ya Vital’O ya Burundi imehamishia mechi yao ya nyumbani wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa Chamazi Complex.

 

Hii ni kutokana na Burundi kukosa uwanja ulioidhinishwa kwa ajili ya mechi za CAF. Mabingwa wa hao wa Ligi Kuu bara msimu uliopita wamepangwa kuvaana na Vital’O FC ya Burundi kwenye mchezo wa hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo Yanga itaanzia ugenini lakini itacheza mechi zote mbili ndani ya ardhi ya Tanzania.

 

Mchezo wa mkondo wa kwanza unatarajiwa kupigwa Agosti 16-18 katika dimba la Benjamin Mkapa huku mkondo wa pili ukipigwa Agosti 23-25 mwaka huu katika dimba la Azam Complex, Chamazi.

Related Posts