Hata hivyo, ili kuondokana na hali hiyo, watu wanatakiwa kuwa na moyo wa imani, kuwepo kwa ushirikiano, kukamata waganga wasio na vibali, elimu iongezwe kwenye jamii, makanisa na misikiti yasiyo na mafundisho mazuri yadhibitiwe , malezi bora na kuwakumbusha watoto wajibu wao, vyombo vya dola kutimiza majukumu yake na kuwalinda wanaotoa taarifa za vitendo hivyo.
Hayo wameyaeleza Wadau wa Jinsia na Maendeleo Julai 24,2024 Jijini Dar es Salaam katika Semina za Jinsia na Maendeleo zinazofanyika kila Jumatano katika Viwanja Vya TGNP- Mtandao huku ikihusisha wadau mbalimbali wa Maendeleo.
Akizungumza katika Semina hiyo, Hamisi Masanja Mkazi wa Manzese amesema kwa sasa ushirikiano kutoka kwenye vyombo vya ulinzi wa raia na mali zao ni mdogo kwani ushirikiano huo ungekuwepo masuala haya ya utekaji wa watoto usingekuepo.
Ameongeza kuwa ni vyema kikosi cha polisi kifanye kazi yake na wananchi kutoa ushirikiano pale utekaji unapitokea.
“Kitu kikitendeka kwanza kitilie hamu kukifahamua kama unaona kinahitaji msaada toa msaada hatakama wa kupiga kelele ili kuokoa maisha yale muhusika” amesema Masanja
Naye Mpegwa Noa kutoka Makulumla amesema masuala ya utekaji wa watoto wazazi wengi wanalalamika hivyo ameiomba serikali kufatilia watekaji hao na kuwachukulia sheria stahiki ili kukomesha mauaji na utekaji ambao umeenea katika baadhi ya maeneo nchini.
Aidha ameiomba serikali kuongeza ulinzi mashuleni na kuwataka wazazi na walimu kushirikiana kuhakikisha mtoto anafika shuleni anakabidhiwa mwalimu na mtoto atakapotoka shuleni akabidhiwe mzazi ili kukomesha vitendo vya utekaji.
Kwa upande wake Afisa Programu Sera kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania, Rogathe Loakaki alisema kama mtandao wa kijinsia Tanzania wanaamini katika hizo sauti za wengi kwani zitawasaidia kudai hatua stahiki ziweze kuchukuliwa na uwajibikaji kwa wale ambao wanasababisha vitendo hivyo lakini pia kuweza kupata sapoti kutoka kwa wadau wengine hasa serikali ambao ndiyo wanasimamia vyombo vya maamuzi kwa nchi na vyombo vya ulinzi.
“Mambo makubwa yaliyoibuka ni hatua mbalimbali ambazo tumekubaliana kuchukua ikiwemo kuweza kufanya tafiti shirikishi, tumeweza kutoa madodoso ili waweze kutoa mawazo yao na pia kuwashirikisha wanajamii wenzao na tuweze kupata tawimu za uhalisia kama kweli tatizo hili lipo kwenye jamii na kwa kiasi gani”
“Katika miaka 25 ijayo vitendo kama hivi hativitaki kwahiyo tumetumia fursa hii tunakoelekea kwenye maandalizi ya dira hii kupaza sauti kwamba dira inapotengenezwa izingatie usalama kwa jamii nzima asiwepo yoyote ambaye atakatiliwa hasa makundi ya wanawake na watoto” ameeleza Rogathe.
Pamoja na hayo amesema TGNP kwa pamoja watashirikiana na serikali pamoja na vyombo vya ulinzi ili waelewe kwamba jamii ni jicho gani wanalo juu ya suala hilo la utekaji wa watoto nchini.