WIMBO WA BEYONCE KUTUMIKA KWENYE KAMPENI ZA KAMALA HARRIS – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

Kampeni ya Kamala Harris ya kuwania urais ilipata msaada mkubwa kutoka kwa Beyoncé, kwa kutumia moja ya vibao vikubwa vya mwimbaji huyo.

 

Kamala alifanya ziara yake ya kwanza rasmi katika makao makuu ya kampeni yake huko Wilmington, Delaware, Jumatatu usiku, wakati akiingia na wimbo maarufu wa Beyoncé, “Freedom” uliotoka mwaka 2016, miaka nane iliyopita.

 

Mtu wa karibu na Harris aliiambia CNN kuwa timu yake ilipokea idhini ya awali kutoka kwa Bey kucheza wimbo huo.

 

Hiyo imekuwa kubwa kwa sababu Beyoncé anaulinda muziki wake na ana sheria kali juu ya kutoa ruhusa kwa mtu yeyote kutumia kazi yake.

 

Lakini kwa Kamala ruhusa ya kuitumia ‘Freedom’ ya Bey ilipita bila kutarajiwa, inasemekana ndani ya saa chache baada ya ombi la timu ya Harris Beyoncé aliwapa ruhusa ya kucheza wimbo huo wa Freedom.

 

Inaonekana kama Beyoncé yuko upande wa Kamala, ingawa hajatoka kuliidhinisha hilo wazi, lakini labda ni suala la muda tu, kwa upande wa Mama wa Beyonce, Tina Knowles, tayari amempa Kamala ndio yake.

 

 

Kama unavyojua, Kamala alichukua nafasi ya Rais Joe Biden baada ya Joe kutoa kauli ya kutoendelea na ugombea wa Uraisi.

Related Posts