ZAIDI YA WAGENI 2000 KUSHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA WAHASIBU WAKUU WA SERIKALI BARANI AFRIKA


Na.Vero Ignatus,Arusha

Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa kimataifa wa wahasibu,wakaguzi wa hesabu,wataalam wa masuala ya fedha,Tehama,vihatarishi na kada nyingine wakiwemo walioajiriwa serikalini,kampuni binafsi pamoja na waliopo katika ajira binafsi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Aicc Jijini Arusha Mhasibu Mkuu wa serikali CPA Leonard Mkude amesema kuwa mkutano huo unatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 2000,ambapo utawaleta pamoja wahasibu wakuu wa serikali Afrika watakaoambatana na wahasibu wakuu wa wizara ,Taasisi za umma ,wahasibu na wadau wengine .

‘’Wahasibu na wakaguzi wa hesabu watakaohudhuria watapata fursa ya kusikiliza mada za masuala mbalimbali ya kitaaluma pia kukutana na wahasibu wakuu wa serikali wa Afrika na kubadilisha na mawazo kupeana mawasiliano na kujua fursa zinazopatikana katika nchi za frika’’.alisema Mkude.

Mkude amesema kuwa mkutano huo utaafanyika nchini kuanzia tarehe 2 hdi 5 Disemba mwaka 2024 katika kituo cha mikutano cha kimatifa Arusha (AICC)huku lengo la mkutano huo likitajwa kuwa ni Kujenga Imani katika Mifumo ya Usimamizi wa Fedha za Umma kwa ukuaji Endelevu.

‘’Ujo huo wa wageni kutoka nje wataleta fedha za kigeni mbazo watazitumia hapa nchini Tanzania katika kuunga mkono dhamira ya Rais ya kutangaza utalii wa Tanzania kwani wageni hawa watatembezwa katika mbuga za wanyama na vivutio mbalimbali’’ alisema CPA Mkude.

Ameainisha faida mbalimbali za mkutano huo kuwa ni pamoja na Afrika yenye mafanikio yenye msingi wa ukuaji jumuishi na maendeleo endelevu,Bara jumuishi lililoungnishwa kisiasa na kwakuzingatia maadili,Afrika yenye utawala bora,Amani na Usalama,Utambulisho thabiti wa kitamaduni,urithi wa pamoja maadili yanayoshirikishwa.


Akizungumza Mwenyekiti wa wa Umoja wa wahasibu wakuu wa Afrika ndugu Mahehlohonolo Mahase amesema kuwa hawachachagua kwa bahati mbaya mkutano huo ufanyike Nchini Tanzania kwasababu ni nchi kinara katika matumizi sahihi ya mifumo,pia mshirika mwaminifu wa umoja huo,vilevile kuna vivutio vingi vya utalii na watu wengi wamekuwa wakisikia tu hivyo wanatamani kuja kuyaona yale ambayo wamekuwa wakiyasikia.

Mahase amesema kuwa umoja wao ni mzuri ambao unalenga kuzisaidia nchi wanachama katika masuala mazima ya kutafuta rasilimali fedha na kuangalia namna gani rasilimalifedha hizo zitatumika katika maendeleo ya nchi husika.
 

Kwa upande wake mkurugenzi wa kituo cha AICC Christine Mwakatobe alisema kuwa wamejipanga vilivyo kuwapokea wageni wa mkutano mkuu wa pili wa wahasibu wakuu wa Afrika na kuhakikisha kuwa wanatoa huduma bora huku wakitegemea kwamba wageni watakapoondoka watarudi tena kutokana na huduma waliyoitoa kwao.

Mwakatobe amemshukuru Dkt Samia kwa kazi kubwa aliyoifanyaa kwani yeye ni mwanadiplomasia namba moja ambao umezaa matunda makubwa kwani wameona mikutano mingi inakuja kwenye kumbi zao ,vilevile utalii umeongezeka pamoja na wawekezaji wameongezeka,pamoja na fursa mbalimbali zilizopo.

Aidha Umoja huo wa wahasibu wakuu wa serikali Afrika ulizinduliwa rasmi Mombasa ,Kenya tarehe 5 julai 2023 bada ya azimio la kufunga umoja wa wahasibu uliokuwepo katika kanda mbalimbali kwa sasa nchi 55 za umoja wa Afrika ni mwanachama wa Umoja huo.

Related Posts