Dr Mwinyi ahimiza Malezi bora katika Jamii

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj. Dk. Hussein Ali Mwinyi amehiwahimiza Wazazi na Walezi kuhakikisha wanasimamia malezi bora yenye maadili kwa watoto na vijana ili kunusuru taifa kuwa na mporomoko wa maadili.

Alhaj. Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo 26 Julai 2024 wakati alipojumuika na waumini wa dini ya Kiislamu katika ibada ya sala ya Ijumaa, msikiti wa Sheikh Sharahan Meli Nne Unguja.

Rais Dk. Mwinyi amesema ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha anasimamia malezi ya watoto na vijana kutokana na mabadiliko ya utandawazi, kwani vijana hujifunza mengi kupitia mitandao ya kijamii.

📍Msikiti wa Sheikh Sharahan, Meli Nne, Unguja

.
.
.
.
.
.

 

Related Posts