Utawala wa Biden umeweza kuiondoa Marekani kutoka kwenye mdororo wa kiuchumi baada ya janga la maambukizi ya Uviko na kupunguza kiwango cha ukosefu wa ajira kwa asilimia 3.4 kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa katika nusu karne. Ukosefu wa ajira ulikuwa asilimia 6.4 wakati Biden na Harris walipoingia madarakani mnamo mwaka 2021. Kiwango kiliendelea kubakia chini ya asilimia 4 kwa muda wa zaidi ya miaka miwili. Hicho ni kipindi kirefu zaidi tangu miaka ya 60.
Kutokana na kupigwa jeki na kitita cha dola trilioni 1.9, ustawi wa uchumi imara ulichepua utashi wa ajira na kuwafanya waajiri kuongeza mishahara. Mishahara ya wafanyakazi wa malipo ya chini ilipanda kwa haraka na hivyo kuweza kupunguza pengo kati ya mapato ya juu na ya chini.
Scholz asema Harris anaweza kushinda uchaguzi Marekani
Hata hivyo misongamano katika mfumo wa ugavi ilisababisha uhaba, wakati ambapo palikuwapo utashi mkubwa wa bidhaa kadhaa ikiwa pamoja na samani na magari.Pamoja na hayo vita vya Ukraine vilichochea bei za nishati na chakula. Mnamo mwezi Juni, mwaka 2022 mfumuko wa bei ulifikia kiwango cha juu kabisa kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha mwongo mmoja.
Ongezeko la bei lilimeza nyogeza za mishahara ya wafanyakazi na hatua hiyo iliwakasirisha wananchi. Ununuzi wa mahitaji ulishuka miongoni mwa wateja mwishoni mwa mwaka 2021 na hali bado haijabadilika japo kiwango cha mfumuko wa bei kilipungua sana kutoka asilimia 9.1 hadi asilimia 3.
Trump anatumia suala la kupanda gharama za maisha katika kampeni yake
Pana tofauti kubwa kati ya taswira hasi ya uchumi miongoni mwa wananchi, na ile chanya ya takwimu juu ya ajira, kupungua kwa mfumuko wa bei na ustawi wa uchumi. Mkuu wa utafiti wa maoni wa asasi ya masuala ya kijamii, Chris Jackson amesema, ni kweli kwamba watu wana ajira na kwamba wanaendelea kupata mishahara, lakini hawaoni iwapo fedha zao zinawafikisha mbali. Jackson amesema watu wa Marekani hawaoni iwapo nchi yao inaelekea kuzuri.
Donald Trump atafanya mkutano wake wa kampeni huko Michigan
Rais wa hapo awali Donald Trump analitumia kwa nguvu zote suala la kupanda gharama za maisha katika kampeni yake. Aliyataja maneno “mfumuko wa bei” mara 14 katika hotuba aliyotoa wakati wa mkutano wa kitaifa wa chama chake cha Republican. Idara ya Hazina ya taifa imesema hadi kufikia mwezi uliopita, kasi ya mfumuko wa bei nchini Marekani ilikuwa ndogo na hivyo kupunguza mfumuko wa bei hatua ambayo itaiwezesha wizara ya fedha kuanza kupunguza viwango vya riba katika msimu huu.
Mwenyekiti wa idara ya Hazina nchini Marekani Jerome Powell amesema mfumuko wa bei unaendana na malengo ya benki kuu ya kiwango cha asilimia 2%.
Amesema viwango vya chini vya riba, mfumuko mdogo wa bei, pamoja na hali thabiti katika soko la ajira, vinaweza kuwafanya wamarekani kuwa na tathmini nzuri ya uchumi wa nchi yao na hivyo Makamu wa Rais Kamala Harris yuko katika nafasi nzuri ya kuyatumia mafanikio ya kiuchumi ya mtangulizi wake Rais Joe Biden kama mtaji wa kisiasa na kuweza kuwashawishi wapiga kura katika kampeni za kinyang’anyiro cha urais kwenye uchaguzi wa mwaka huu kati yake na Rais wa zamani Donald Trump.