Ligi Kigoma kuamsha Agosti 8

LIGI za Kikapu kwa mikoa mbalimbali zinazidi kushika kazi kwa sasa, huku ile ya Mkoa wa Kigoma ikitarajiwa kufanyika Agosti 8.

Katibu Mkuu wa Chama cha Kikapu Kigoma, Aq Qassim Anasi, amesema kwa upande wao wamepanga ligi hiyo ianze Agosti 8 na maandalizi yanaendelea vizuri hadi sasa.

Akizungumza na Mwanaspoti kwa simu kutoka Kigoma, Anasi alisema timu tano ndizo zilizothibitisha   kushiriki Ligi hiyo ya Mkoa kwa mwaka huu.

Alitaja timu hizo ni; Tanganyika BC, Lake Side, Spide, Kasulu na Kibondo na kuongeza kuwa, wanasubiri kupata timu nyingine kama idadi itaongezeka hata moja tu, basi watazigawa timu hizo katika makundi mawili yenye timu tatu tatu ili kurahisisha mambo kwa hatua ya mtoano.

“Kama timu zikibakia timu tano, mfumo utakaotumika kila timu itacheza na mwenzake,” alisema Anasi, aliyeomba pia wadau mbalimbali wa mchezo huo na wengine kujitokeza kudhamini Ligi hiyo ya Kigoma.

Related Posts