Mwabukusi ashinda rufaa, sasa kuwania urais TLS

Dar ES Salaam. Mahakama Kuu imetengua uamuzi wa Kamati ya Rufaa ya TLS uliomwengua kwenye kinyang’anyiro cha kugombea urais wa chama hicho cha Wanasheria wa Tanganyika

Uamuzi huo ambao umetolewa leo Julai 26, 2024 na Jaji Butamo Phillip, ndio unaotoa hatima ya Mwabukusi katika kinyang’anyiro hicho.

Mwabukusi alikuwa mmoja wa wanachama walioomba na kupitishwa na Kamati ya Uchaguzi kugombea nafasi ya urais wa TLS, lakini akapingwa kwenye kamati ya maadili ambayo ilimwengua.

Uchaguzi wa TLS unatarajiwa kufanyika Agosti 2, 2024 jijini Dodoma.

Endelea kufuatilia Mwananchi

Related Posts