Mziki wa Dube, Baleke ni moto! Gamondi afunguka amtuliza Mzize

KOCHA Miguel Gamondi anashindwa kujizuia na kuchekelea kimtindo namna washambuliaji wapya wa timu, Prince Dube na Jean Baleke walivyoanza maisha ndani ya timu hiyo, akisema namna bora ya wao kujitambulisha ni kufunga mabao.

Baleke na Dube kila mmoja amefunga bao katika mechi mbili tofauti zilizopita za kirafiki za kimataifa timu ikiwa Afrika Kusini, hatua ambayo imemtuliza Gamondi, aliyetegemea zaidi viungo washaumbuliaji katika michuano ya msimu uliopita.

Baleke alifunga bao la kufutia la machozi la Yanga ilipoumana na FC Augsburg ya Ujerumani, huku Dube juzi aliipa timu hiyo ushindi mbele ya TS Galaxy ya Afrika Kusini, kila mmoja akiingia kipindi cha pili cha mechi hizo zilizokuwa za michuano maalumu ya Mpumalanga International Cup.

Akizungumza na Mwanaspoti, Gamondi alisema Baleke na Dube wameanza vizuri ambapo haijalishi muda ambao amekuwa akiwapa wamekuwa wakifanya kitu kinachotakiwa.

Gamondi alisema hatua ya kwanza ambayo inamtambulisha mshambuliaji mzuri ni kufunga mabao ambayo wote wawili wameifanya ambapo sasa anataka kuona wanaongeza kutumia nafasi zaidi.

“Nafurahia namna wanavyojituma Baleke (Jean) anajituma sana angalia namna alivyofunga katika mechi ya FC Augsburg, pia anapambana uwanjani kujiweka maeneo sahihi ya kufanya kitu bora,” alisema Gamondi na kuongeza;

“Vivyo hivyo pia kwa Dube angalia muda ambao amekuwa akipewa, lakini anajituma kufanya kitu sahihi, jana (juzi) amefunga bao zuri, kwangu mimi mshambuliaji anajitambulisha kwa kufunga kama wanavyofanya lakini wanatakiwa kuendeleza kasi ya kutumia nafasi zaidi.”

Akimzungumzia mshambuliaji Clement Mzize, kocha Gamondi alisema bado hana shida ya kinda huyo na kwamba ana mambo mengi mazuri anayafanya kuliko kupimwa kwa kutumia nafasi.

“Siku zote nasema watu wasimuangalie Mzize kwa kutumia nafasi pekee, huyu ni kijana ambaye tunaendelea kumtengeneza zaidi lakini kuna mambo mengi makubwa anayafanya uwanjani ambayo mashabiki wanaweza wasiyaone,” alisema.

  ndio maana mnaona tunaendelea kumtumia,” alisema Gamondi akimzungumzia mshambuliaji huyo aliyemaliza na mabao sita ya Ligi Kuu na matano ya Kombe la Shirikisho jinsi anavyopoteza nafasi za kuifungia timu mabao.

Related Posts