VILABU VINAVYOSHIRIKI MICHEZO YA MEI MOSI WAHIMIZWA KULIPA ADA YA USHIRIKI KWA WAKATI

 

Na Mwandishi wetu

 

Taasisi
na Mashirika ambayo yana malimbikizo ya ada za ushiriki wa michezo ya
wafanyakazi zimeombwa kulipia ada ya ushiriki mapema ili kufanikisha
michezo hiyo inayofanyika kila mwaka wakati wa Siku Kuu ya Wafanyakazi
Duniani, Mei Mosi.

 

Rai
hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Mei Mosi Taifa
Roselyne Mathew Massam kwenye kikao cha Viongozi Vilabu vya michezo
ambvyo vipo kwenye Mashirikisho ya Michezo nchini ambao wamekutana
kufanya tathimini ya michezo hiyo iliyofanyika mwezi Aprili mwaka huu
Jijini Arusha.

 

Massam,
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma
(SHIMUTA), amesema kuwa ucheleweshaji wa ulipaji wa ada unakwamisha
ufanisi wa michezo hiyo na kusababisha kushindwa kugharimia gharama za
michezo hiyo ikiwemo kulipia viwanja vizuri vyenye ubora.

 

Massam
amesema Kamati hiyo ya Michezo ya Mei Mosi inaundwa na mashirikisho ya
SHIMIWI, SHIMUTA, SHIMISEMITA na BAMATA ambapo katika tathimini hiyo
kamati hiyo imeweka mkakati wa kuongeza timu zitakazozoshiriki
mashindano hayo mwakani ambapo mwaka huu Jumla ya timu 56 zimeshiriki
ukilinganisha na timu 33 zilizoshiriki mwaka jana 2023.

 

Amesema
kuwa Kamati imekuwa na utaratibu wa kufanya tathimini ili kutambua
changamoto zilizojitokeza zisijirudie tena hivyo kuboresha michezo ijayo
iwe mizuri zaidi.

 

Massam,
amesema kamati hiyo inaendelea kuhamasisha Wizara, Idara, taasisi,
mashirika ya umaa na sekta binafsi kuhakikisha kila mfanyakazi anafanya
mazoezi na kushiriki michezo hiyo kwa ajili ya kuimarisha afya.

 

Katibu
Mkuu wa Kamati ya Michezo Taifa Alex Faustini Temba, ameishukuru
Serikali kwa kutoa kibali kwa wafanyakazi kushiriki michezo hiyo ambapo
mbali na kucheza michezo hiyo tofauti tofauti walichanga fedha shilingi
milioni 13, ambazo walizitoa kwa Vituo vya wahutaji jijini Arusha.

 

Naye
Mwenyekiti wa Michezo Shirika la Viwango Nchini (TBS), Nyabuchwenza
Methusela, amesema michezo ya mwaka huu ilikuwa na mafanikio licha ya
changamoto iliyojitokeza ya uchelewaji wa washiriki kuhudhuria na hivyo
kuathiri ratiba na kusababisha michezo kuchezwa mfululizo asubuhi na
jioni.

 

Related Posts