Wenyeviti wa Baraza la Vijana Zanzibar wafanya hili Wilaya ya Micheweni Pemba

Wenyeviti wa Baraza la Vijana Zanzibar wakiongozwa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo wamesema wameridhishwa na Miradi inayojengwa na kusimamiwa na Serekali ya awamu ya nane katika Wilaya ya Micheweni Pemba.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana Taifa Salum Issa Ameir wakati akuzungumza na Waandishi wa Habari katika Ziara ya Wenyeviti wa Mabaraza ya Vijana ya Zanzibar ikiwa na lengo la Ukaguzi wa Miradi ya kimkakati katika Kisiwa cha Pemba.

Amesema kukamilika kwa Miradi hiyo itakwenda kuzalisha Ajira kwa Vijana wa Micheweni na Pemba kwa Ujumla.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Micheweni Is-haka Khamis Makame amesema Micheweni inakwenda kupiga hatua kubwa kimaendeleo pamoja na kuwataka wananchi kulinda miundombinu hiyo.

Nae Dakari dhamana wa hospital ya Wilaya ya Micheweni amesema ujio wa hospital katika Wilaya hiyo kumeleta mafanikio makubwa katika sekta ya Afya.

.
.
.
.

Related Posts