AFARIKI KWA KUKANYAGWA NA TEMBO – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Mwanaume mmoja anayeitwa Lowasa Kimaa mwenye umri wa miaka 54 ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Makame Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, amefariki dunia huku taarifa zikitaja kuwa alikanyagwa na tembo.

 

Akiongea na vyombo vya habari, Ijumaa Julai 26, 2024 Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara RPC George Katabazi amesema kuwa Marehemu alikutwa na umauti baada ya kukanyagwa na tembo wakati akisafiri kwa pikipiki akiwa na mwenzake na kwamba Kimaa ndiye alikuwa dereva aliyekodishwa kupeleka abiria katika Kijiji cha jirani Orkiushibour kilichopo Kata ya Ndedo Tarafa ya Makame ambapo ndipo alipovamiwa na tembo aliyemkanyaga na kupoteza maisha.

 

Kamanda Katabazi ameeleza kuwa watu hao ambao ni jamii ya kifugaji ya Maasai huishi kwenye hifadhi ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA) ambayo ina wanyama wengi kama vile tembo na nyati, huku akiwataka wananchi hao kuchukua tahadhari kwa wanyama hao wakali akiwaasa kutotembea nyakati za usiku ili kuepukana na tukio kama hilo lililotokea.

 

Related Posts