Aweso aweka kambi Singida kutafuta suluhu Maji chini ya Ardhi

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso ameipongeza Kampuni ya AL FRADAWS investment Company Limited kutoka Jordan ambayo ni wawekezaji katika uzalishaji wa Mbegu mbalimbali Mkoani Singida kwa Kuja na Suluhisho katika Upatikanaji Maji Mkoani humo Kupitia Teknolojia ya Pivot irrigation System.
Mkoa wa Singida ni kati ya mikoa yenye changamoto ya vyanzo vya Maji vya uhakika na upatikanaji maji chini ya ardhi.

Akizungumza wakati alipotembelea Kampuni iliyopo Kijiji cha Choda wilayani Ikungi leo tarehe 27 Julai 2024 Waziri Aweso Amesema Teknolojia ambayo inatumiwa na Kampuni ya FRODAWS ni nzuri kwa kuwa inatoa majibu ya uhakika katika Utambuzi wa maeneo yenye maji kabla ya kuanza shughuli za uchimbaji.

Lengo la ziara hiyo ambayo imehusisha utafiti wa vitendo kwa njia ya anga kwa kutembelea maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mji wa Kiomboi Singida ni kuona namna gani teknolojia hiyo inavyoweza kutumika katika maeneo mbali mbali Nchini ili kutatua tatizo la maji.

.
.
.

Related Posts