Klabu ya Kristiansund BK ya Norway wameandika barua kwa Simba SC wakimuomba Kibu Denis kwa majaraibio, wamekiri kwamba hawakuambiwa ukweli kuhusiana na mchezaji hali iliyopelekea wao kufanya makosa ya kuwasiliana na kumtumia mwaliko mchezaji mwenye mkataba unaozidi miezi 6 bila kwanza kuwasiliana na klabu na kupata ruhusa kuwaliana na mchezaji na kumtumia huo mwaliko. Wamekiri pia kukiuka taratibu na kanuni za FIFA na wameiona hatari iliyopo mbele yao.
Simba SC wao wako tayari kumuachia Kibu Denis aondoke ila wanataka kipengele cha kuuzwa mchezaji kifikiwe tu ambacho ni dola za Kimarekani milioni 1 ($1M) ambacho ni sawa na bilioni 2.7 za Kitanzania (Tshs 2.7B).
Hawataki kusikia kuhusu majaribio kwakuwa kuna kukosa na kupata, ikitokea akakosa na kurudi manake watakuwa wametoa mwanya kwa wachezaji wao kuondoka kihuni.
Kristiansund BK wao wanaona bilioni 2.7 ni nyingi sana wanataka suluhu na Mnyama amegoma anataka heshima yake iliyopotezwa.
Ingawa uzoefu unaonyesha Simba ni klabu ambayo inaongoza kuwaachia wachezaji kwenda nje kucheza wanapopata nafasi, hata hili pia watafikia mwisho na Kibudenga atapata nafasi kucheza Ulaya na kutimiza ndoto zake.
Imeandikwa na BIN KAZUMARI MTIPA (The voice of the voiceless)