PROF MKENDA AITANGAZA RASMI SAMIA SCHOLARSHIP EXTENDED ILIYOTENGEWA BAJETI YA BILIONI 1.6.

Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolph Mkenda amesema kuwa wamegundua uwepo wa uhaba mkubwa wa wataalam katika nyanja ya Sayansi na Teknolojia ya Nyukilia hapa Nchini ambapo uhalisia unaonesha kuna idadi ndogo ikiwemo Afya,Elimu,Nishati, Viwanda,Kilkmo na kwingineko.

Prof. Mkenda ameyasema hayo leo hii Jijini Dodoma katika mkutano na Wanahabari wakati akitangaza rasmi kuhusu ufadhili huo wa Samia Scholarship Extended wenye lengo la kuendeleza mpando wa kukuza Sayansi,Tehama,Hisabati,Uhandisi,Elimu na fani zilizo kipaumbele cha Taifa.

Katika kuongeza amesema mfano katika sekta ya Afya takwimu zinaonesha kuwa kuna Nyukilia Medicine Doctors 6 tu hapa Nchini, Wataalam wa kutengeneza na kuchanganya madawa ya mionzi wapo 2 tu na Wataalam wa Ekolojia wako chini ya 100 hapa Nchini.

“Sasa tumegundua kuwa tuna uhaba mkubwa sana wa Wataalam katika nyanja ya Sayansi ya Teknolojia ya nyukilia hapa Nchini, uhalisia unaonesha kuwa kuna idadi ndogo sana ya wataalam wa Sayansi na Teknolojia ya Nyukilia katika Sekta mbalimbali ikiwemo Afya,Elimu,Nishati,Viwanda,Kilimo na kwingineko”.

“Mfano katika eneo la Sekta ya Afya tuna Medical Physist 6 tu hapa Nchini, tuna Nyukilia Medicine Doctors 6 tu,Radio Chemistry 1 tu,Wataalam wa kutengeneza na kuchanganya madawa ya mionzi wapo 2 tu Nchini na wataalam wa Ekolojia wapo chini ya 100 hapa Nchini”.

“Katika sekta ya Elimu ambapo tunahitaji kuwa na wahadhili wengi wanaofundisha watu wetu napo tuna uhaba mkubwa ambapo wenye PhD takwimu sasahivi zinaonesha tunao 10 tu,wengine tuliokuwa nao mahiri kabisa wamestaafu mfano wa Dkt Mohamed Gharib Bilal ambaye alikuwa Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kwahiyo tuna upungufu mkubwa sana nyanjia hizo na tunazihitaji sana”.

Aidha Waziri ameeleza kuwa kuanzia mwaka wa fedha wa 2022/2023 Serikali kupitia Wizara ya Elimu ilianza kutoa ufadhili wa asalimia 100 kwa wahitimu wenye ufaulu wa juu katika masomo ya Sayansi kwenye mitihani ya kidato cha sita endapo wahitimi hao watachagua kusoma maosoma ya Sayansi, Tehama,Hisabati,Uhandisi na Elimu Tiba ambapo wameendelea kufanya mfululizo na wanufaika ni wengi.

“Kama mnavyofahamu Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia inatekeleza mpango wa kukuza Sayansi, Tehama,Uhandisi,Hisabati na Elimu Tiba pamoja na fani nyingine za kipaumbele zikiwemo fans ambazo zina wataalam wachache hapa Nchini. Kama mnakumbuka kuanzia mwaka wa fedha 2022/2023 Wizara ilianza kutoa ufadhili wa asilimia 100 kwa wahitimu wenye ufaulu wa juu katika masomo ya Sayansi katika mtihani wa kidato cha sita,endapo tu wahitimu hao watachagua kwenda kusoma masomo ya Sayansi, Tehama,Uhandisi, Hisabati na Elimu Tiba kwa vyuo vya ndani ya Nchi,hayo tumekuwa tukiyafanya mfululizo na wanufaika ni wengi”.

Mbali na hayo pia Waziri ametoa msimamo wa Wizara kwa kushirikiana na Taasisi zake zote kuwa imeamua kuongeza wigo wa Samia scholarship kwa wanafunzi wa kidato cha sita wanaokwenda chuo kikuu ikiwa lengo ni kuhakikisha kwamba wale waliofaulu vizuri katika masomo wanafanya masomo hayo tu na sio kurudi katika masomo mengine yasiyo ya Sayansi.

“Kwahiyo Wizara kwa kushirikiana na Taasisi zake zote imeamua kuongeza wigo wa Samia Scholarship kwa wanafunzi wa kidato cha sita wanaokwenda chuo kikuu na lengo lake ni kuhakikisha kwamba wale waliofaulu vizuri kwenye masomo ya Sayansi hawaondoki kwenda kufanya masomo mengine”.

Naye Prof Najat Mohammed ambaye ni Mkurugenzi wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) katika mkutano huo ametoa maelezo juu ya sifa za mwombaji anazopaswa kuwa nazo ambapo amesema kuwa ni pamoja na kuwa Raia wa Tanzania na asiyezidi umri wa miaka 35,awe muhitimu wa chuo kikuu shahada ya awali kwa kipindi kisichozidi miaka 5 na kuwa na ufaulu wa juu kuanzia kiwango cha GPS ya 3.5 ya 5 au wastani wa ufaulu wa B kwa shahada ambazo hazina GPA.

“Ili kuweza kupata ufadhili wa Samia Scholarship wa shahada ya umahiri wa Sayansi na Teknolojia ya Nyukilia, muombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo”.

“Kwanza awe Mtanzania mwenye umri usiozidi miaka 35, Pili awe maehitimu chuo kikuu shahda ya awali aliyemaliz kipindi kisichozidi miaka 5. Tatu awe na ufaulu wa juu kuanzia kiwango cha GPA ya 3.5 kati ya 5 au wastani wa ufau wa B kwa shahada ambazo hazina GPA,wenye matokeo ya jumla katika shahada ya awali ya Sayansi ya Uhandisi, Hisabati,Tehama,Elimu Tiba, Nishati,Kilimo na fani zingine za kipaumbele cha Taifa”.

Fedha hii ya Shilingi Bilioni 1.6 iliyotengwa ni ya kuanzia walau kwa Watanzania wa tano katika fani zilizoainishwa na kuwepo uhaba wa Wataalam.





Related Posts