TPA TANGA YAPEWA KONGOLE NA TASAC

Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania -TASAC imeipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kutekeleza vema mradi wa uboreshaji wa bandari ya Tanga na kuwezesha meli kufunga ghatini na kuongeza asilimia 30 ya mapato ya bandari ya Tanga.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa Bodi hiyo Nahodha Mussa Mandia wakati akizungumza na vyombo vya habari tarehe 26 Julai, 2024 jijini Tanga ambayo ni siku ya tano tangu bodi hiyo ianze ziara ya ukaguzi wa huduma ya udhibiti zinazofanywa na TASAC.

“Tumevutiwa na utaratibu wa usalama.wa bandari wenye kiwango cha usalama.daraja la kwanza ambavyo ni vigezo vya bandari inayotoa huduma kwa viwango vya kimataifa.Pili tumeona mazingira safi ya bandari na shughuli zinaendeshwa kwa mpangilio mzuri.Tuna kila sababu ya kujivunia utendaji wenu wa kazi na uwekezaji wa Serikali awamu ya Sita inayoongozwana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mhe, Dkt.Samia Suluhu Hassan na kusababisha mapato kuongezeka kwa asilimia 30.Hongera sana uongozi TPA na bandari ya Tanga.” Amesema Nahodha Mussa Mandia.

Bandari ya Tanga ilijengwa tangu mwaka 1888 na mwazo ilikuwa inatoa huduma kwa mzigo kushusha kwenye baji umbali kilomita 1.7 na kukotwa hadi ghatini.Lakini kwa sasa mara baada ya kuboresha meli inakuja moja kwa moja na kufunga ghatini.

Mwenyekiti wa bodi hiyo Nahodha Mussa Mandia amewaasa uongozi wa bandari Tanga kutenga eneo la mizigo michafu na safi, kuendelea ujenzi bandari katika eneo la zaidi mitaa 300 kwa ajili ya kuwa na ghati ya kuhudumia meli au boti za abiria pasipokuingilia na shughuli za ghati zinazohusika kushusha mizigo.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Bwana Mohamed Salum ametoa wito kwa bandari kutenganisha eneo la mizigo hatarishi na mizigo mengine. Pia ametoa wito kwa mawakala wa meli kuanza kuleta meli bandari ya Tanga kwa mizigo inapakuliwa kwa haraka na gharama.nafuu ukilinganisha na zamani walipokuwa wanatumia baji.

Aidha ameongeza bandari iendelee kufanya maboresho na watoa huduma za uwakala wa forodha, wapakiaji mizigo wawe eneo la kufanyia kazi nje ya bandari ili kuongeza ufanisi.
Kwa upande wake Bwana Masoud Mrisha meneja wa bandari ya Tanga amesema kuwa bandari sasa imepata mizigo mipya ya salfa,ammonia na shaba na kuongeza mizigo kufikia zaidi ya ujazo wa tani milioni 100 kwa 2023/24 ukilinganisha na mizigo iliyohudumiwa kwa mwaka 2022/23 ambayo ilikuwa zaidi tani za ujazo zaid ya laki 8.
“Tunashukuru Serikali ya awamu ya sita ya Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania kwa kuwekeza mradi wa uboreshaji bandari wenye zaidi ya bilioni 400 na kusababisha bandari kuwa na ufanisi na kuongeza mapato yatakayosaidia Serikali kutekeleza miradi ya maendeleo.” amesema Bwana Masoud Mrisha.
Mkuu wa Mkoa Mhe.Balozi Dkt.Batilida Burian ameomba TASAC kuendelea kusimamia kwa karibu ili mizigo michafu itenganishe na mizigo mengine pale inapohudumiwa.

“TASAC nawaomba mfanye ukaguzi mara kwa mara na kuwaelekeza TPA watenge ghala ya kufadhia mizigo michafu ya salfa na ammonia” Amesema Mhe.Balaozi na Dkt Batilida.
Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania imendelea kufanya ziara na kugagua eneo la mradi wa ujenzi wa ghati ya kupokelea mafuta ghafi kutoa Huima nchini Uganda kuona hatuna za kiusalama zinafuata wakati huu ujenzi wa ghati hiyo.
Bodi hiyo iliendelea na ziara hadi kituo cha pamoja cha forodha Holoholo ambapo walipokea maoni ya wadau wanaofanyakazi na TASAC katika kuhudumia mizigo inayosafirisha na bahari kupitia bandari ya Mombasa kuja nchini Tanzania au kupitia Bandari ya Tanga na Dar es salaam kwenda nchini Kenya. Wadau wameishukuru TASAC kwa kuendelea kuwapa ushirikiano mzuri na kufanya mnyororo usafiri bahari kustawi.

Related Posts