Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe ametangaza kuachia nafasi hiyo huku akisema muda wake umemalizika.
Kamwe aliyehudumu katika nafasi hiyo kwa miaka miwili amethibitisha kuondoka Yanga kupitia ukurasa wake wa mtandao w Instagram leo Jumapili Julai 28, 2024.
“Mtumbuizaji mzuri anatakiwa kujua ni wakati gani wa kuondoka Jukwaani. Maneno ya hekima kutoka katika kinywa cha Patrick Loch Otieno Lumumba.
“Na ni Hekima hii, inanituma mbele yenu Wananchi, mashabiki na wanachama wa Klabu yetu pendwa, kuwaambia kuwa, Ni wakati sasa wa kijana wenu kuondoka Jukwaani,” ameandika Kamwe.
Kamwe ameongeza kuwa muda wake umemalizika na anawashukuru sana.
Endelea kufuatilia Mwanaspoti kwa taarifa zaidi