MILIONI 500 KUSAIDIA MAJI KWA WAKAZI 10701 TARIME MJINI – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Zaidi ya shilingi Milioni 500 zimetumika katika mradi wa Maji wa Sabasaba ulioko Wilayani Tarime Mkoani Mara ambapo mradi huo unatazamiwa kuhudumia wakazi takribani 10701.

 

 

Akizindua mradi huo wa maji kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Godfrey Mnzava amewataka wananchi kutunza Miradi inayotekelezwa na Serikali ili kuendelea kuwa na manufaa kwa wananchi ambapo pia ameipongeza taasisi ya Ruwasa kutekeleza maaagizo ya serikali kuhusu matumizi ya mfumo wa NEst.

 

 

Kwa upande wake meneja wa Ruwasa Wilaya ya Tarime Mhandis Mohamed Mtopa amesema kwa sasa mkakati uliopo nikuongeza Mtandao wa Maji kwa Wananchi ili kuhakikisha Mradi huo unakuwa na manufaa kwa wananchi.

 

 

Baadhi ya wakazi wa mtaa huo wameishukuru Serikali kukamilisha mradi huo ambapo sasa umesaidia kuondoa matumizi ya Maji ya mito ambayo hayakuwa Safi na salama.

 

Related Posts