Dar es Salaam. Waumini wa Kanisa la Christian Life Church linaloongozwa na Mchungaji Domique Kashoix Dibwe, maarufu Kiboko ya Wachawi, lililopo Buza Kwa Lulenge, jijini Dar es Salaam wakiimba wimbo wa kuwa na imani na mchungaji wao baada ya kanisa kufungwa.
Waumini hao wamefika kanisani hapo asubuhi ya leo Jumapili Julai 28, 2024 licha ya kuwa huduma zimesitishwa, lakini wameendelea kusalia makundi makundi huku wengine wakifanya maombi kabla ya kuanza kupinga uamuzi huo.
Barua ya kufungiwa kwa kanisa hilo imetaja sababu ni kwenda kinyume cha taratibu za usajili.
Barua hiyo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Ofisi ya Msajili wa Jumuiya za Kiraia ya Julai 25, 2024 ambayo Mwananchi imeiona iliwaelekeza Mwenyekiti wa Kanisa la Christian Life Church na Mchungaji Dibwe kufunga tawi la kanisa hilo lililopo eneo la Buza kwa Lulenge, Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Endelea kufuatilia mitandao ya kijamii ya Mwananchi