BREAKING; SNURA ATANGAZA KUACHA MUZIKI, AKATAZA NYIMBO ZAKE KUCHEZWA POPOTE – MWANAHARAKATI MZALENDO

#BURUDANI Aliyekuwa Msanii wa Muziki wa Bongofleva na Muigizaji , Snura Mushi ametangaza rasmi kuacha muziki na kuamua kumcha Mungu baada ya kufanya kazi hiyo kwa takriban miaka kumi. Snura ametanga uamuzi huo leo July 29,2024 ingawa hakutaka kuweka wazi ila imembidi ili kuondokana na kadhia ya wafuasi na umma kumuhusisha na masuala ya sanaa tena.

“Watanzania na nje ya nchi mimi Snura leo natangaza rasmi kuwa nimeacha kazi za sanaa nilizokuwa nazifanya. Sababu kubwa ya kuacha ni kumrudia muumba wangu, nifuate dini yangu ya Kiislamu inavyosema na mwanamke wa Kiislamu anavyotakiwa kuwa,” Snura

“Nisingeweza kupita kila redio na Tv kuwakataza wasicheze nyimbo zangu, natumia fursa hii ndugu zangu kwa heshima na taadhima naomba sana mnipokelee ombi langu msicheze kazi zangu kabisa naomba mfute, fanyeni kama hakuna kilichotokea,” Snura.

“Ukisikia nimekufa umehuzunishwa na msiba wangu njoo unizike kama ni mwanamke usije mtupu njoo na stara, picha ambazo hazina heshima msiposti hayo mapicha wala madude dude kwa sababu naona tukifa hayo madude ndiyo mnaposti,” Snura

Unamshauri nini Snura kuhusiana na uamuzi aliouchukua? 

#KonceptTvUpdates

Related Posts