Kagoma afichua ndoto ya udaktari ilivyomezwa na soka

NAMBA 21 mgongoni iliyokuwa inatamba dimba la kati katika kikosi cha Singida Fountain Gate msimu wa 2024/25, msimu ujao tutarajie kuiona Simba.

Sio mwingine ni kiungo fundi mzawa panga pangua chini ya makocha wote waliopita Singida Fountain Gate, Yusuf Kagoma ambaye amesema anatamani kutumia namba hiyo akiwa na timu yake mpya.

Spoti Mikiki limefanya mahojiano na Kagoma ambaye amekiri alikuwa na wakati mgumu pindi ali-potuhumiwa kusaini Simba na Yanga kwa wakati mmoja.

“Haikuwa rahisi mambo yalikuwa ni mengi lakini ukweli nilikuwa naujua mimi. Yanga sikusaini kama watu walivyokuwa wanasema bali walileta ofa kama ilivyo Simba.

“Mara baada ya Simba kunitangaza kuwa mchezaji wao kidogo nilipumua kwani hilo hata mimi nilikuwa nalisubiri kwa hamu ili kuepukana na changamoto za simu nyingi sambamba na maoni mengi ya wadau,” anasema Kagoma.

Kagoma anasisitiza kuwa alisaini upande wa Simba tu.

“Mimi ndio nilikuwa nafahamu ukweli wa mambo lakini ni kweli nilikuwa na ofa kutoka Yanga ambao ndio walikuwa wa kwanza kunifuata na Simba baadae wakaweka ofa mezani nafikiri walikuwa na uhitaji kweli kwani walifanya mambo kwa haraka,” anasema kiungo huyo.

Licha ya mastaa wengi wa kigeni kutua Tanzania wakitoa changamoto kwa mastaa wa wazawa, Kagoma amesema hakuna utofauti wa ubora baina ya viungo wazawa na wageni 

“Tanzania imebarikiwa kuwa na vipaji vya wachezaji wengi hasa nafasi ya kiungo hata ukifuatilia Ligi Kuu Bara unaweza kukubaliana na mimi kwani wachezaji wengi wanaofanya vizuri ni nafasi ya kiungo.

“Pamoja na timu kubwa kuwa na wachezaji wa kigeni kwenye nafasi hizo bado wanawachanganya na wazawa ambao pia wameonyesha uwezo mkubwa na wa kuvutia huku wakitajwa zaidi midomoni mwa wa-tu,” anasema Kagoma.

Anasema utofauti upo kwasababu binadamu wanatofautiana anaweza kuwa na kitu mguuni na mwingine akakosa lakini kwa asilimia kubwa wazawa wameamka na kuonyesha kuwa wanaweza.

Kagoma anasema siri ya washambuliaji wengi kutofanya vizuri ni kuridhika.

“Waafrika ni wepesi wa kuridhika hii ndio sababu kubwa ya washambuliaji wetu wengi kushindwa kuwa na muendelezo wa ubora lakini uwezo wanao lakini wakishafunga mabao yao kumi wanaona wamesha-maliza.

“Washambuliaji wengi wa kizawa wakipata mafanikio msimu mmoja, unaofuata huo ni wakiendeleza kile walichokifanya msimu uliopita hii ni kwasababu wanaridhika,” anasema Kagoma.

KIUNGO HADI BEKI ANACHEZA

Nyota huyo wa zamani wa Geita Gold anasema kuwa anamudu kucheza kiungo na beki.

“Nimezoeleka na kufahamika sana kutokana na kutumika zaidi kucheza nafasi ya kiungo lakini mimi ni mchezaji ambaye nimepata nafasi ya kucheza nafasi tatu uwanjani na zote kwa ubora.

“Naweza kucheza kwa ubora kabisa nafasi ya beki wa kati na beki namba mbili ni nafasi ambazo nimepata nafasi ya kucheza nikiwa kwenye kikosi ambacho kinashiriki Ligi Kuu Bara sio kwamba nimecheza nikiwa madaraja ya chini,” anasema Kagoma.

Kagoma anafichua kuwa amecheza timu nne tofauti za ligi kuu kwa misimu nane.

“Nimeanza kucheza Singida United ikiwa daraja la kwanza na baadaye ikapanda nikacheza misimu miwili. Baafa ya kushuka niliondoka na kujiunga ni timu nyingine lakini ni moja ya timu ambayo nimecheza misimu mingi zaidi.

“Baada ya kutoka Singida United nilijiunga na Gwambina ambayo niliitumikia kwa miaka miwili uwezo niliouonyesha nikiwa na timu hiyo ndio uliwavutia Geita Gold ambao walinichukua na kunisainisha mkataba wa miaka miwili lakini nimewatumikia mwaka mmoja na nusu na baada ya hapo ndipo nilipo-chukuliwa na Singida Big Stars ambayo nimeitumikia hadi mwisho wa msimu na wameniuza Simba,” alisema Kagoma.

Kagoma anafichua kuwa alikuwa na ndoto za kuwa daktari lakini hazikutimia kwa sababu ya soka.

“Ndoto yangu ilikuwa ni kuwa daktari nakumbuka tangu naanza shule nikiulizwa unasoma ili uwe nani ji-bu lilikuwa ni kuwa Daktari ili niweze kuwatibu wagonjwa.

“Lakini soka lilichukua nafasi kubwa zaidi ya masomo pamoja na kufanikiwa kumaliza kidato cha nne lakini sikuweza kutimiza ndoto yangu na kujikuta nawekeza nguvu zaidi kwenye mpira ambao pia nilikuwa naupenda,” anasema kiungo huyo.

Kagoma anamtaja Felix Minziro kama miongoni mwa makocha bora waliowahi kumnoa

“Nimepita chini ya makocha wengi lakini kocha Fredy Felix Minziro’ni kocha ambaye pamoja na ubora wake kwenye majukumu yake ni kocha ambaye anafurahia kazi na vijana wake wawapo uwanjani.

Related Posts