NCHIMBI AWAPONGEZA MTWARA VIJIJINI UTEKELEZAJI ILANI YA CCM

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiambatana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, ameendelea na ziara yake ya mikoa miwili ya Kusini, Lindi na Mtwara leo tarehe 29 Julai 2024 amepata fursa ya kuzungumza na Wananchi wa Jimbo la Mtwara Vijijini, Kata ya Mpapura.

Akiwa hapo Mpapura, Balozi Nchimbi amesema pamoja na kwamba jimbo hilo linaongozwa na mbunge asiyekuwa wa CCM, lakini Ilani ya Uchaguzi inayotekelezwa ni ya CCM, ambapo aliwapongeza wanachama na viongozi wa CCM na wananchi, kwa kushirikiana na Serikali ya CCM, kuhakikisha ilani hiyo inatekelezwa kwa kiwango cha juu.

Ameongeza kusema kuwa hilo limefanikiwa kwa sababu Mbunge wa CCM Jimbo la Nanyamba, Mhe Abdallah Chikota anafanya kazi pia ya kuwa kaimu mbunge kuwawakilisha na kuwasemea wananchi wa Mtwara Vijijini.

“Hapa hakika kazi Imefanyika nafikiri mmeona sasa kazi kwenu wakati ukifika inadili mbadilike kwani pamoja na yote CCM inawafanyia mambo makubwa tumeyasikia hapa wenyewe sasa wakati ukifika pigeni chini wasiobadilika kichagueni Chama cha Mapinduzi.”

Mwisho amewaasa wananchi kuendelea kutunza na kulinda amani na utulivu na wasikubali kadanganywa na mtu yeyote kuhusu kuharibu tunu hiyo adhimu.

Balozi Nchimbi pia amechangia Shilingi 10 milioni kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Ofisi ya CCM Wilaya ya Mtwara Vijijini.

Mapema kabla, Katibu Mkuu wa CCM Balozi Nchimbi alikutana na Kamati ya Siasa ya CCM ya Mkoa wa Mtwara kwa ajili ya kikao na kupokea taarifa ya utendaji wa kazi wa CCM na utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi ya Mwaka 2020 – 2025, kutoka kwa uongozi wa Chama na Serikali mkoani humo.



Related Posts