Picha: Mabingwa wa vifaa vya kielectonic ‘Haier’ wazindua tawi lao Mkoani Mwanza

Ni Headlines za Mabingwa wa vifaa vya kielectronic ‘Haier’ wamezindua tawi lao litakalokuwa likipatikana Rock City Mall Gorofa ya kwanza Mkoani Mwanza.

Sasa Kwa wakazi waishio maeneo ya jirani Mkoani humo wakifika kwenye Mall hiyo wataweza kujipatia bidhaa mbalimbali za kieletronic ikiwemo TV, Friji, Majiko na Jezi mpya za Young Africans Msimu wa 2024/25.

Kampuni ya Haier iliingia rasmi ubia na kampuni ya GSM GROUP mnamo mwanzoni mwa mwaka 2023. Kwa kipindi hiki chote, kampuni ya Haier ikishirikiana na GSM GROUP imekuwa ikihakikisha inaleta bidhaa ambazo zina tija sokoni.

‘Tangu uanzishwaji wa kampuni ya Haier, Tanzania, tumekuwa tukijitahidi kuangalia matakwa ya soko na kuhakikisha tunaboresha huduma na ufanisi wa bidhaa zetu kwa watumiaji’ Alisema haya meneja biashara, Bw. Ibrahim Kiongozi.

 

.
.
.
.
.
.
.
.

Related Posts