Rais Samia amteua Katungu bosi mpya wa Magereza

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Kamishna wa Magereza, Jeremiah Katungu kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) na kumteua kuwa Mkuu wa Jeshi la Magereza.

Uteuzi huo umetangazwa leo Jumatatu, Julai 29, 2024 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, ikimnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka ikieleza kuteuliwa kwa Katungu kuchukua nafasi ya CGP Mzee Nyamka aliyestaafu.

Nyamka ameliongoza Jeshi la Magereza kwa siku 705, sawa na mwaka mmoja na miezi 11, kuanzia Agosti 24, 2022, alipoteuliwa.

Katungu anakuwa Kamishna wa Jeshi la Magereza wa 17 kushika wadhifa huo. Baada ya kupatikana kwa Uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 9, 1961, Jeshi la Magereza liliendelea kuongozwa na Kamishna wa Magereza Muingereza, Patric Manley hadi mwaka 1962 jeshi hilo lilipoanza kuongozwa na wazalendo.

Related Posts