URUS TZ teknolojia ya uhiilishaji mifugo maenesho Nanenane

IKIWA ni sehemu ya kusaidia jitihada za kukuza sekta ya mifugo hapa nchini, Kampuni ya URUS inatatajiwa kushiriki maonesho ya Nanenane mwaka huu katika mikoa sita ya Morogoro, Dodoma, Mbeya, Arusha, Simiyu na Kagera kwa lengo la kuonyesha teknolojia ya kisasa na yenye tija zaidi ya uzalishaji wa mifugo kupitia uhimilishaji kutoka nchini Marekani na Brazil. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).

URUS Tanzania, ni kampuni tanzu ya URUS global yenye makao makuu yake nchini Marekani, ambayo pamoja na mambo mengine, inajishughulisha na usambazaji wa mbegu bora za ng’ombe wa maziwa na nyama duniani.

Takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania ni nchi ya pili barani Afrika kwa wingi wa mifugo baada ya Ethiopia lakni mkakati mabadiliko na kukuza sekta ya mifugo 2022/23-2026/27 unaonyesha kuwa sekta hii inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwa na pamoja na matukizi ya mbegu za kionyeji zinazotoa uzalishaji mdogo wa maziwa na nyama.

Meneja mkazi wa URUS Tanzania, Edson Mfuru alisema kampuni hiyo inashiriki maonesho ya Nane nane ili kuonyesha teknalojia ya kisasa ya uhimilishaji kutoka Marekani na Brazil ambazo zinaweza kuwa na mchango mkubwa katika kukuza sekta ya mifugo kwa kuongeza uzalishaji.

“Lengo letu ni kusaidia kuongeza uzalishaji wa bidhaa za mifugo kama nyama na maziwa kupitia teknalojia rahisi,rafiki na yenye ufanisi ya uhimilishaji. Teknalojia tunayoitumia inawezesha kupatikana kwa ng’ombe chotara wa nyama na maziwa wenye uwezo wa kuzalisha maziwa zaidi pamoja na nyama kuliko ng’ombe wetu wa kienyeji,”

Meneja huyo aliesema teknalojia hiyo tayari imeshaanza kutumika hapa nchini na kuongeza kuwa baadhi ya wafugaji wamenufaika nayo huku jitihada zaidi zikifanyika kuwafikia wafugaji katika sehemu mbalimbali.

“Wafugaji watutembelee katika maonesho ya Nane nane na tutakuwepo Morogoro, Dodoma, Mbeya, Arusha, Simiyu na Kagera ili waweze kujifunza zaidi kuhusu teknalojia hii pamoja na kupatiwa huduma,” alisema.

About The Author

Related Posts