YANGA YAMREJESHA ALLY KAMWE KATIKA NAFASI YAKE – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Rais wa klabu ya Yanga, Mhandisi Hersi Said na Makamu wake Arafat Haji wamesema kuwa rasmi Meneja wa idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ally Kamwe amerudi kazini na anaendelea na majukumu yake.

 

Viongozi hao wametoa taarifa hiyo leo Julai 29, 2024 katika mkutano na Waandishi wa habari uliofanyika Jangwani kariakoo jijini Dar es Salaam ambapo wameeleza kuwa Kamwe alieleza changamoto zake kwa uongozi ambazo zilimpelekea kuchukua uamuzi wa kujiuzulu kwa maslahi ya pande zote mbili na uongozi umekubali kuzifanyia kazi.

 

 

“Tumefanikiwa kumrejesha kazini Ally Kamwe kwenye nafasi yake ya Meneja Habari na Mawasiliano na tayari amesaini mkataba mpya wa miaka miwili ndani ya klabu’’, amesema Injinia Hersi

 

 

Ikumbukwe kuwa jana Julai 28, 2024 Ally Kamwe alitoa taarifa ya kujiuzulu nafasi hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Related Posts