Raisa Said,Handeni
Watanzania wamehamasishwa kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan ili aweze kutekeleza na kukamilisha miradi ya maendeleo inayotekelezwa.
Rai hiyo imetolewa na Mdau wa Maendeleo Handeni Mariam Mwanilwa wakati akizungumza na wanawake zaidi ya 200 walioshiriki tamasha la wanawake lijulikanalo kama Handeni Woman Handeni lililofanyika ukumbi wa Makuti.
” Rais Dk Samia anafanya kazi kubwa usiku na mchana kuhakikisha tunapata maendeleo, sisi kama wananchi jukumu letu ni kumuunga mkono pamoja na kumuombea ili miradi ikamilike kwaajili ya maendeleo yetu.” Alieleza Mwanilwa mdau huyo wa maendeleo.
Alisisitiza kuwa agenda yao kwasasa kama wanawake ni kuhakikisha 2025 wanakwenda na Rais Dk Samia Suluhu Hassa,nakwamba mwanamke namba moja ni Samia Suluhu Hassan kwakuwa amekuwa mstari wa mbele kutetea haki za wanawake.
Pia Mwanilwa alieleza juu ya umuhimu wa kuzingatia malezi ya watoto wao huku akiwataka wanawake wasijikite sana katika kutafuta pesa pekee na kusahau malezi ya watoto kwasababu kumekuwa na mmomonyoko wa maadili katika jamii.
” Sisi ndio walezi wa familia na tunajukumu la kulea familia zetu tunatakiwa tubadilike ili kupambana na mmomonyoko wa maadili katika jamii zetu” Alisema Mwanilwa huku akiongeza kuwa tusiwachie ulezi wa watoto wetu wafanya kazi wa ndani pekee .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Handeni Women galla Mwajuma lisu amesema kuwa lengo la kufanya tamasha hilo la handeni women galla ni kutaka kuwainua wanawake kiuchumi lakini pia ni kutaka kumuunga mkono Rais Samia namna anavo wakwamua wanawake kiuchumi.
Lisu alisema handeni women galla ina lengo la kutaka wanawake wajifunze na waweze kufanya shughuli zao bila kikwazo chochote pamoja na kuwapa elimu ili waweze kutatua changamoto zao.
Hata hivyo katika Handeni women galla mada mbalimbali zilitolewa ambapo mada hizo ni Malezi,Ndoa na Mahusiano,Afya ya akili,Mwanamke na uongozi,Ujasiriamali na biashara Afya ya uzazi, Akiba na mikopo pamoja na Masuala ya sheria