GSM atangaza rasmi kinywaji kipya, Yanga SC apata Shavu la kukitangaza…

Ni July 30, 2024 ambapo GSM Group of Companies leo wanayofuraha ya kupanua wigo wa mahusiano na Klabu ya Yanga ambapo wametangaza rasmi kampuni yao mpya ya vinywaji ya GSM kuingia mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo.

“Kwa niaba ya GSM Group tunayo furaha ya kutangaza rasmi kuwa tumepanua wigo wa mahusiano yetu na klabu ya Yanga SC, tunatangaza rasmi kuwa kampuni mpya ya vinywaji ya GSM imeingia mkataba wa miaka mitano na klabu ya Yanga SC, na mkataba huu una thamani ya Tsh bilion 1” Benson Mahenya CEO wa GSM Group

“Tunashukuru sana Uongozi wa GSM Group kwa kutambua umuhimu wa kuongeza nguvu ya udhamini kwa klabu yetu, Kampuni hii ya vinywaji visivyo na kileo kama juisi, soda na maji itakuwa sehemu ya wadhamini wetu kwa kipindi hicho cha miaka mitano” Simon Patrick – Mkurugenzi wa Sheria wa Klabu ya Yanga SC

.

Aidha Mkurugenzi wa Sheria Klabu ya Yanga SC, Simoni Patrick amesema ….“Leo tumekuja hapa kuwatangazia wadhamini wetu kuelekea kilele cha wiki ya Mwananchi, mdhamini mkuu wa wiki ya mwananchi ni benki ya CRDB, hata hivyo tumeongeza washirika wengine ni Benki ya Equity pamoja na GSM Beverage”

 

Related Posts