Kupotea watoto kwaisukuma E.A.G.T Temeke kufanya maombi maalumu

Na Winfrida Mtoi

Kanisa la Evangelistic Assemblies of God  (E.A.G.T), Temeke linatarajia kufanya semina na maombi maalumu  kuliombea Taifa, viongozi pamoja na kuomba  ili kuondokana na tatizo la watoto kupotea.

Semina hiyo inatarajiwa kufanyika Agosti 4 -11,2024, viwanja vya  Temeke Chang’ombe jijini Dar es Salaam, huku neno kuu likiwa ‘ Yote Yanawezekana kwa Mungu Wetu’.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 30, 2024, Mchungaji wa Kanisha hilo Christomoo Ngowi, amesema maombi hayo pia yatahusu vijana kutokana na kuporomoka kwa maadili na vijana wengi kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya.

“Sasa hivi mabadiliko yanayotokea ni makubwa hali ni mbaya vijana wameharibika,  wanatumia dawa za kulevya, si sheria zinaweza kuwarudisha katika maadili  bali ni Mungu mwenye uwezo wa kubadilisha tabia ya mtu,” amesema  Mchungaji  Ngowi.

Amewakaribisha watu  wa dini zote katika semina hiyo  ambapo kutakuwa na waimbaji kama vile John Lissu, Joel Lwanga, Boaz Danken na kwaya  nyingine ikiwamo ya kanisa hilo.

Related Posts