MGALU AKABIDHI VYEREHANI 11 VYENYE THAMANI YA MIL.3.3 KWA UWT MAFIA ILI KUJIINUA KIUCHUMI

Na Mwamvua Mwinyi,Mafia – PWANI

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mhe. Subira Mgalu amekabidhi vyerehani kumi na moja (11), vyenye thamani ya Tsh. 3,300,000/- kwa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) wilayani Mafia, kwa lengo la kuwawezesha kiuchumi.

Vyerehani hivyo amevitoa ikiwa ni ahadi yake aliyoiahidi wilayani humo, na amelenga kuwanyanyua kiuchumi wanawake wa Jumuiya hiyo katika Kata zake zote nane.

“Fani ya ushonaji inaongoza kwa kipato, wakijipanga watafanikiwa,” Mhe. Mgalu amesema.

Aidha, ametoa rai kwa Jumuiya hiyo wasigombane, na washirikiane kwa kuwa amewapa vyerehani hivyo kwa umoja wao kwa ajili ya kujiwezesha wenyewe, ili kuwezesha shughuli za UWT katika wilaya hiyo.


Related Posts