Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), DK. Emmanuel Nchimbi leo alasili atahutubia mkutano mkubwa wa hadhara kwenye Uwanja wa Mpilipili Mjini Lindi.
Asubuhi atafanyiwa mapokezi rasmi katika Ofisi za CCM za Mkoa huo, ambapo atafanya kikao na Kamati ya siasa na baadaye mkutano wa ndani wa viongozi wa chama wa Mkoa huo
Lengo la ziara hiyo ni; Kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020, kuhuisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki Taarifa zao na kujiandikisha katika kitabu Cha kudumu Cha Wapiga kura, kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba mwaka huu.
Katika ziara hii Dk Nchimbi amemaliza ziara ya siku mbili mkoani Mtwara, ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amosi Makalla, Katibu wa NEC-Organaizesheni Ndg. Issa Ussi Haji (Gavu) pamoja na Katibu wa NEC- Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Rabia Abdallah Hamid.