Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Sekta binafsi ina mchango wa kizalendo wa maendeleo wa kuhakikisha Tanzania inazidi kupiga hatua na kwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi .
Dkt Mwinyi aliyasema hayo wakati wa Mkutano wa 15 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Julai 2024.
Aidha Rais Dkt.Mwinyi amesema Maazimio ya mkutano wa 15 wa Baraza la Taifa la Biashara yatakuwa ni dira kutatua changamoto zinazokabili shughuli za biashara nchini na kuwa mwongozo kwa Serikali, watendaji na wafanyabiashara katika kufungua ukurasa mpya wa mageuzi ya kidijiti .
Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) kwa umahiri wa uongozi wake wa kukuza uchumi nchini .
#KonceptTvUpdates