Tukio hilo lilitokea Alfajiri ya Julai 29, na kusababisha watoto kutembeakilomita kadhaa kutafuta maeneo salama kunusuru maisha yao. DW ilifuka katika eneo la tukio umbali wa kilomita 18 kusini mashariki mwa Kalemie na kujionea hali ilivyo.
Hali ya kufuka kwa moshi katika baadhi ya nyumba ndivyo vilivyopata nafasi kuwa katika eneo hilo. Mamia ya raia wakiwemo wanawake na watoto wamekimbia Kijiji hicho kwa kutembea kwa miguu kilomita nyingi wakielekea mji wa Kalemie na vijiji jirani.
Ombi kwa serikali ya Kongo kuwalinda raia
Katika tukio hilo watu watatu akiwemo askari jeshi mmoja waliuwawa na wengine wanane walijeruhiwa kwa mishali. Tumbwe Mwamba Celestin ni kiongozi wa kijiji hicho ameitolea wito serikali kuimarisha usalama
Shirika la kutetea raia NDSCI kupitia makamu kiongozi wao Byaesse Issa wameiomba serikali kurejesha usalama katika vijiji mbalimbali jimboni humo kwani matukio mengi yametokea mwezi huu
Chama Mukalay raia mwenye huzuni ambae amekutwa amekaa mbele ya nyumba yake iliyoungua ameionyooshea kidole cha lawama serikali.
Serikali yataka wananchi warejee katika makazi yao
Waziri wa mambo ya ndani na ulinzi jimboni humuo Dieudonne Kasaka ambaye alikuwepo kwenye eneo la tukio, amethibitisha vifo vya watu hao na kuomba raia warejee katika kijiji hicho kwani ulinzi umehimarishwa
Raia wanaendelea kuwalaumu askari jeshi kwa kile wanachosema ni kutokuwajibika ipasavyo kwenye matukio ya mara kwa mara kwenye Vijiji kadhaa. Jeshi la taifa FARDC jimboni Tanganyika kupitia msemaji wao John Munta wamedai jumla ya nyumba 2750 zimeunguzwa na wamewaomba raia kuliamini jeshi hilo.
Soma zaidi: Rais Tshisekedi ana nadi sera zake Tanganyika
Rekodi zinaonesha kuwa watu takribani 10 wameuawa ndani ya siku zisizo zidi 15 huku 7 miongoni mwao wakiuwawa kwa kuchinjwa katika vijiji vya Mutenta, na Tabac Congo.
DW kalemie