FAINI YA TZS 104 KWA WANAOTUMIA MIUJIZA KUWATAPELI WANANCHI – MWANAHARAKATI MZALENDO

Serikali ya Kenya inapanga kuwachukulia hatua kali viongozi wa kidini wanaotumia udanganyifu kufanya miujiza, uponyaji, au kutoa baraka ili kuwaibia raia. Mapendekezo haya, yakipitishwa, yatamlazimisha kiongozi wa kidini kulipa faini ya Ksh. 5 milioni (TZS milioni 104.7) au kifungo cha miaka kumi gerezani, au vyote viwili.

Kikosi Kazi cha Rais kuhusu Mapitio ya Mfumo wa Kisheria na Udhibiti wa Mashirika ya Kidini kimewasilisha Muswada wa Mashirika ya Kidini wa mwaka 2024, unaoweka hatua kali dhidi ya viongozi wa dini wanaowaomba waumini kutoa pesa kwa ajili ya baraka au mafanikio kifedha.

Muswada huo pia unaadhibu viongozi wanaotumia nguvu au vitisho kuwalazimisha watu kujiunga na dini zao kwa faini ya Ksh. 1 milioni (TZS milioni 20.9) au kifungo cha miaka mitatu gerezani, au vyote viwili.

Aidha, mtu yeyote atakayetumia dini kudharau imani ya mtu mwingine na kutishia usalama wao atatozwa faini ya Ksh. 5 milioni au kifungo cha miaka 20 gerezani, au vyote viwili. Kikosi kazi pia kimependekeza makanisa yasijihusishe na siasa, na yakivunja sheria, yatatozwa faini ya Ksh. 500,000 (TZS milioni 10.5) au kifungo cha miezi sita gerezani, au vyote viwili.

#KonceptTvUpdates

Related Posts