KADA CHADEMA AHAMIA CCM, KUUNGA MKONO JUHUDI ZA MAENDELEO – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

Mtemi Lushumkono Maige Tito Aliyekuwa Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa muda mrefu kutoka Kata ya Igurubi, Jimbo la Igunga Ameamua kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kile alichokisema kuwa ‘hakuna Chama mbadala wa CCM ‘ katika kuleta maendeleo na ustawi wa Taifa.

 

 

 

Mtemi Lushumkono Maige Tito Amepokelewa kupitia Mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe. Nicholaus George Ngassa uliofanyika Makao Makuu ya Tarafa ya Igurubi kwenye Viwanja vya Soko la Igurubi.

 

 

 

Mtemi Lushumkono Maige Tito amekipongeza Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kazi kubwa ya kuboresha huduma za jamii na kusema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kinara wa maendeleo na wao kama Sungusungu watamuunga mkono bila kuchoka.

Related Posts