Kama unataka kufanya biashara ya usafiri wa mtandaoni chagua magari haya

Watu wengi wanaotaka kuanza kufanya biashara ya usafiri wa mtan­daoni hujiuliza kuhusu aina za magari zitakazofaa katika kuleta faida kubwa zaidi kwenye biashara hii ya usafirish­aji.

Hii ni muhimu kwa madereva ambao tayari wanaendesha abiria wa usafiri huo kwa sababu, dereva anaweza kubadili gari muda wowote na kuweza kutengeneza pesa zaidi.

Katika makala haya tutazungum­zia baadhi ya magari yanayofaa kwa biashara hii ambayo yatakusaidia kupata faida kutokana na gharama zake za uendeshaji.

Aina nyingine ya gari dogo lenye muonekano mzuri na nafasi ya kuto­sha ni Toyota Spacio. Magari haya pia yapo mengi kwenye majukwaa ya usafiri wa mtandaoni Tanzania kwa sababu yanapatikana kwa bei nzuri.

Aina hii ni ndogo zaidi ukilingani­sha na Spacio hivyo pia bei yake ni ndogo zaidi. Ukubwa wa injini yake pia ni 1496 cc.

Toyota Raum zinatumia petroli, tenki lake lina uwezo wa kujaza lita 52 na utumiaji wake wa mafuta ni Lita moja kwa wastani wa kila Km 15.

Aina nyingine ya gari dogo na lin­alopendwa kutumiwa na madereva katika majukwaa usafiri wa mtandaoni ni Toyota Passo. Size yake ndogo muon­ekano ni mzuri na ni rahisi kuegesha sehemu yoyote.

Muonekano wa gari aina ya Passo. Picha na Mtandao

Size na muundo mzima wa aina hii ya Toyota husaidia matu­mizi madogo ya mafuta hivyo kuongeza uwezo wa kupata faida kubwa zaidi katika biashara.

Hii ni moja kati ya aina ya magari yaliyopo kwa wingi zaidi Tanzania. Hii ni kwa sababu bei yake ni nzuri na utumiaji wake wa mafuta ni mdogo. Lita moja ya mafuta inaweza kupele­ka gari umbali wa Km 11.5 na tanki la mafuta lina uwezo wa kujaza Lita 42.

Muonekano wa gari aina ya IST. Picha na Mtandao

Ukilinganisha Toyota IST na Toyota Vitz, yote yana size nzuri, yanatumia mafuta kidogo na idadi ya siti ni sawa lakini, Vitz hutumia mafuta kidogo zaidi. Hii inamaanisha kuwa aina hii ni nzuri kwa ajili ya biashara ya usafiri kwa sababu dereva anakuwa na gharama ndogo ya uendeshaji gari hivyo kupelekea faida kubwa zaidi. Lakini ukilinganisha kwa kutumia kigezo cha starehe, Toyota IST zina nafasi kubwa zaidi ya Toyota Vitz.

Madereva wengi wanatumia aina hii ya gari katika kusafirisha abiria kwenye majukwaa ya usafiri wa mtan­daoni. Aina hii ina bei nzuri, inatumia mafuta kidogo na modeli nyingine zina muonekano fulani kama wa magari ya mashindano ambao huvu­tia watu wengi.

Changamoto za kutumia magari haya

Ingawa magari haya yana faida nyingi na yanafaa kwa biashara, bado yana mapungufu ambayo huenda yanasababisha kupungua kwa ufanisi wake wa kutoa huduma. Changamoto kubwa ni pamoja na;

Magari haya ni mafupi, kwa hiyo huleta shida kwa dereva ikitokea amepita sehemu zenye mashimo na pia yana uwezekano wa kuharibika mara kwa mara kutokana na kugonga chini.

Moja ya sababu kuu inayopelekea magari haya kutumia mafuta kidogo ni uzito na nafasi yake ndogo. Kiti cha mbele inaweza kuwa na nafasi kubwa zaidi kwa ajili ya kunyoosha miguu kuliko za nyuma ila haishauriwi kwa abiria kukaa mbele.

Related Posts