Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma, ametembelea mradi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa Arusha kukagua maendeleo ya mradi huo.
Ktika ziara hiyo, Waziri Mwinjuma alieleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi na kujitolea kwa mkandarasi katika kutekeleza maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuiandaa Tanzania kwa AFCON 2027. Alisisitiza kuwa mkandarasi ameahidi kukamilisha mradi kwa wakati licha ya kuchelewa kidogo.
Wakati wa ziara hiyo, Mwinjuma aliona wananchi wengi wakijipatia ajira moja kwa moja kupitia ujenzi wa mradi huu, akibainisha kuwa wanatambua umuhimu wa kazi wanayofanya kwa ajili ya maendeleo ya nchi. Mwakilishi wa mkandarasi kutoka kampuni ya CRCEG, Gregory Mbuya, alithibitisha kuwa mradi huo utachukua miezi 24 kukamilika, na kazi za maandalizi zinaendelea vizuri.
Aidha, ziara ya Waziri Mwinjuma imeonesha dhamira ya serikali kuhakikisha miundombinu ya michezo inaboreshwa na kuwa tayari kwa mashindano makubwa kama AFCON.
#KonceptTvUpdates