Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha, kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania, limemkamata Samwel Mbise (42), mkazi wa Sanawari, Arusha, kwa kufanya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni pasi na kibali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo, ametoa taarifa hiyo leo, Julai 31, 2024. Amesema kuwa mtuhumiwa alikamatwa katika operesheni inayoendelea iliyoanza Julai 29, 2024, na alikutwa na fedha mbalimbali.
SACP Masejo alifafanua kuwa mtuhumiwa huyo alikutwa na Dola za Marekani 5,952, Euro 835, Dola za Canada 1,845, Pound 45, Switzerland Franc 20, Dola za Australia 50, Qatar Riyals 05, Pound za Egypt 25, Shilingi za Kenya 38,400, na Shilingi za Tanzania 52,552,000. Jumla ya fedha hizo ni Shilingi milioni 75,809,649 za Kitanzania.
Jeshi la Polisi linaendelea na msako kuhakikisha wahalifu wote wanaojihusisha na biashara hii wanakamatwa na kuchukuliwa hatua stahiki kisheria.
#KonceptTvUpdates