TANZANIA, MALAWI NA MSUMBIJI KUSHIRIKIANA KUTUNZA NA KUENDELEZA BONDE LA MTO RUVUMA

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maji imeingia mkataba wa makubaliano na Ushirikiano na nchi ya Malawi na Msumbiji kuweka mikakati ya pamoja katika utunzaji, ulinzi na uendelezaji wa Bonde la Mto Ruvuma.

Makubaliano hayo yamesainiwa leo Julai 31,2024 jijini Dar es Salaam ambapo Tanzania imewakilishwa na Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso upande wa Malawi wamewakilishwa na Waziri wa Maji Mhe. Abida Sidik Mia na nchi ya Msumbiji ikiwakilishwa na Waziri wa Maji Mhe. Carlos Mesquita.

Akizungumza katika hafla hiyo , Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema kupitia mshirikiano hayo, nchi hizo tatu zitaungana katika ulindaji na utunzanji wa vyanzo vya maji kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo ili waendelee kupata maji safi na salama.

“Nchi yetu ya Tanzania tumekuwa na mito mingi, sasa baadhi ya mito unakuta inapita katika baadhi ya nchi zingine hivyo suala la ulindaji na utunzaji wa vyanzo vya maji lazima liwe endelevu”

“Faida yake ni kwamba mto Ruvuma baina ya nchi hizi tatu tutaweka macho yetu katika ulindaji na utunzaji hivyo utakuwa na manufaa kwa vizazi vya sasa na vijavyo katika kuhakikisha unakuwa endelevu na watanzania waendelee kupata maji safi na salama” amesema Mhe. Aweso

Aidha Waziri Aweso amewataka wadau mbalimbali wa maendeleo, taasisi na sekta zote kujitokeza ili kusaidia jitihada hizo zilizoanzishwa huku akisisitiza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan yuko tayari kuhakikisha ushirikiano huo unaendelelea kuimarishwa.

Kwa upande wa Waziri Sidik Mia kutoka Malawi amesema mafanikio ya usalama wa bonde la Mto Ruvuma ni heshima kwao na vizazi vijavyo hivyo lazima wote kwa pamoja wahakikishe kazi hiyo inafanikiwa, huku Mhe. Carlos Mosquita wa Msumbiji akisisitiza umoja na kuwataka Wananchi na wadau wote kutoa ushirikiano.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji-Wizara ya Maji na Mwenyekiti wa Kamati ya Wataalamu ya Bonde la Mto Ruvuma, Bw. George Ligombela amesema hati ya makubaliano hayo inawezesha ushirikiano wa nchi hizo tatu kuanzisha sekretarieti ya Bonde la mto Ruvuma itakayokuwepo katika mji wa Mtwara ambapo kutakuwa na watumishi kutoka nchi zote tatu.

Amesema kupitia mpango shirikishi wa usimamizi wa Rasilimali za maji katika bonde la Ruvuma, MoU hiyo imetilia mkazo katika kutekeleza kwa pamoja mashirikiano hayo.

Pamoja na hayo amesema wataanzisha majukwaa ya wadau wa nchi zote ambayo yatahusisha wadau kutoka nchi ya Msumbiji, Malawi na Tanzania ili kujadili namna gani changamoto za usimamizi wa rasilimali za maji katika bonde hili limatatuliwa.

Waziri wa Maji nchini Tanzania , Mhe. Jumaa Aweso (wa kwanza kushoto), Waziri wa Maji nchini Malawi Mhe. Abida Sidik Mia na Waziri wa Maji nchini Msumbiji, Mhe. Carlos Mesquita wakisaini mkataba wa makubaliano na ushirikiano baina ya nchi hizo tatu kuweka mikakati ya pamoja katika utunzaji, ulinzi na uendelezaji wa Bonde la Mto Ruvuma. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 31,2024 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Maji nchini Tanzania , Mhe. Jumaa Aweso (wa kwanza kushoto), Waziri wa Maji nchini Malawi Mhe. Abida Sidik Mia na Waziri wa Maji nchini Msumbiji, Mhe. Carlos Mesquita wakisaini mkataba wa makubaliano na ushirikiano baina ya nchi hizo tatu kuweka mikakati ya pamoja katika utunzaji, ulinzi na uendelezaji wa Bonde la Mto Ruvuma. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 31,2024 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Maji nchini Tanzania , Mhe. Jumaa Aweso (wa kwanza kushoto), Waziri wa Maji nchini Malawi Mhe. Abida Sidik Mia na Waziri wa Maji nchini Msumbiji, Mhe. Carlos Mesquita wakisaini mkataba wa makubaliano na ushirikiano baina ya nchi hizo tatu katika kuweka mikakati ya pamoja katika utunzaji, ulinzi na uendelezaji wa Bonde la Mto Ruvuma. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 31,2024 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Maji nchini Tanzania , Mhe. Jumaa Aweso (wa kwanza kushoto), Waziri wa Maji nchini Malawi Mhe. Abida Sidik Mia na Waziri wa Maji nchini Msumbiji, Mhe. Carlos Mesquita wakionesha mkataba waliosaini wa makubaliano na ushirikiano baina ya nchi hizo tatu katika kuweka mikakati ya pamoja katika utunzaji, ulinzi na uendelezaji wa Bonde la Mto Ruvuma. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 31,2024 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Maji nchini Tanzania , Mhe. Jumaa Aweso (wa kwanza kushoto), Waziri wa Maji nchini Malawi Mhe. Abida Sidik Mia na Waziri wa Maji nchini Msumbiji, Mhe. Carlos Mesquita wakipongezana mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano na ushirikiano baina ya nchi hizo tatu katika kuweka mikakati ya pamoja katika utunzaji, ulinzi na uendelezaji wa Bonde la Mto Ruvuma. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 31,2024 Jijini Dar es Salaam. 

Waziri wa Maji nchini Tanzania , Mhe. Jumaa Aweso akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano na ushirikiano baina ya nchi tatu (Tanzania, Malawi na Msumbiji) katika kuweka mikakati ya pamoja katika utunzaji, ulinzi na uendelezaji wa Bonde la Mto Ruvuma. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 31,2024 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Maji nchini Malawi Mhe. Abida Sidik Mia akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano na ushirikiano baina ya nchi tatu (Tanzania, Malawi na Msumbiji) katika kuweka mikakati ya pamoja katika utunzaji, ulinzi na uendelezaji wa Bonde la Mto Ruvuma. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 31,2024 Jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Bi. Agnes Meena akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano na ushirikiano baina ya nchi tatu (Tanzania, Malawi na Msumbiji) katika kuweka mikakati ya pamoja katika utunzaji, ulinzi na uendelezaji wa Bonde la Mto Ruvuma. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 31,2024 Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji-Wizara ya Maji na Mwenyekiti wa Kamati ya Wataalamu ya Bonde la Mto Ruvuma, Bw. George Ligombela akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano na ushirikiano baina ya nchi tatu (Tanzania, Malawi na Msumbiji) katika kuweka mikakati ya pamoja katika utunzaji, ulinzi na uendelezaji wa Bonde la Mto Ruvuma. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 31,2024 Jijini Dar es Salaam.





Baadhi washiriki wakiwa katika hafla ya utiaji saini mkataba wa makubaliano na ushirikiano baina ya nchi tatu (Tanzania, Malawi na Msumbiji) katika kuweka mikakati ya pamoja katika utunzaji, ulinzi na uendelezaji wa Bonde la Mto Ruvuma. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 31,2024 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Related Posts