UDSM Outsiders vichapo kiduchu | Mwanaspoti

Wakati Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) ikiendelea katika Uwanja wa Donbosco Osterbay, timu ya UDSM Outsiders inaongoza kwa kufungwa pointi chache.

UDSM inayoshika nafasi ya pili katika msimamo wa BDL imefungwa pointi 821 ikifuatiwa na Dar City iliyofungwa 987.

Timu zingine ni ABC iliyofugwa pointi 893, JKT ABC (893), Savio (1021) Mgulani JKT (1068), Mchenga Star (1091), Vijana ‘City Bulls’ (1120), Chui ( 1149) na Jogoo (1172).

Zingine ni KIUT (1279), Pazi (1291), DB Oratory (1329), Srelio (1336) na Crows (1381).

Kwa upande wanawake JKT Stars imefungwa pointi 678 ikifutiwa na Tausi Royals iliyofungwa 696.

Related Posts